Hii ndio Bodaboda iliyogonga gari dogo aina ya Suzuki Escudo katika barabara ya Segerea Kinyerezi mapema Mchana wa Leo na Kupelekea tafrani ambapo waendesha bodaboda walimshushia kipigo dereva wa gari dogo aina ya Suzuki kwa Kumuita Mwizi.
Wanausalama Wa kituo Cha Staki Shari Wakimsikiliza Dereva wa gari dogo aina ya Suzuki Escudo (Mwenye Fulana Nyeusi) akielezea jinsi alivyogongwa na muendesha Bodaboda na bahati mbaya walivyomgeuzia kibao na Kumpa kipigo hadi kupelekea dereva huyo kuumia Vibaya hususani sehemu ya jichoni.
Askari wa Jeshi la Polisi Kutoka Kituo Cha Stakishari akimpeleka Dereva Wa Gari Dogo aina ya Suzuki escudo kwenye gari la Polisi tayari kwa kuelekea nae kituoni na kutoa maelezo jinsi maswahibu yalivyompata.
Mwendesha bodaboda ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa ndani ya pingu huku akitoa maelezo kwa Askari polisi kwanini alimuita dereva wa gari dogo mwizi na kupelekea bodaboda wenzie kumpiga dereva huyo na kumsababishia maumivu na majeraha wakati dereva huyo wa bodaboda ndie aliyegonga gari dogo hilo aina ya suzuki escudo.
Dereva bodavoda akisubiria amri kutoka kwa Wanausalama hao wakati walipofika kutuliza ghasia ambazo zingepelekea dereva wa gari dogo aina ya suzuki kupigwa na dereva wa bodaboda kwa kuitwa mwizi wakati mwenzao ndie aliyegonga gari hilo
Askari Polisi na Raia Mwema wakimpeleka Dereva wa bodaboda kwenye gari la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kutoa maelezo juu ya tukio zima
Dereva bodaboda (mwenye pingu) akiwasikiliza wana Usalama
Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya Segerea Mfaume akikemea tabia za bodaboda kujichukulia sheria mikononi hata kama wao ndio wametenda kosa
Dereva wa Gari dogo aina ya Suzuki Escudo (Wa Kwanza Kushoto) lililongogwa na dereva wa Bodaboda akisubiria kupelekwa Kituo Cha Polisi Cha Stakishari
Hilo ndio Gari aina ya Suzuki Escudo iliyogongwa na dereva wa bodaboda mchana wa leo maeneo ya Segerea
Raia wakishuhudia tukio hilo wakati askari walipowasili kuja kutuliza ghasia
Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog
Dereva wa gari dogo aina ya Suzuki escudo amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kupokea kipigo kutoka kwa waendesha bodaboda baada ya mwenzao mmoja kugonga gari hilo aina ya suzuki escudo na kumbadilishia kesi dereva huyo wa suzuki escudo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Waendesha Bodaboda walikuwa kwenye msafara kuelekea eneo la karibia na stendi ya daladala ya segerea ambapo walikua wanaenda kumkamata mtu mmoja ambaye alimwibia mwenzao pikipiki juzi wakati wakiwa katika Msafara huo mwendesha bodaboda mmoja aligonga gari hilo aina ya Suzuki Escudo wakati likiwa linaelekea pembeni ya barabara kwaajili ya kuegeshwa na kupelekea kudondoka pembeni kama ilivyo kawaida yao waendesha bodaboda hao wakamfuata dereva huyo na kuanza kumpa kipondo huku wakimuita mwizi na hatimaye mashuhuda wa tukip ndipo walipoweza kuingilia kati na kuweza kutuliza kwa muda vurrugu hizo hadi hapo wanausalama walipoweza kuwasili na kumkamata muendesha bodaboda aliyetaka kusababisha mauti kwa dereva wa gari dogo aina ya Suzuki Escudo.
Wakati askari wakiwapeleka mwendesha bodaboda na dereva wa suzuki katika kituo cha Polisi Ndipo walipokutana na waendesha bodaboda wakiwa wanarudi kutoka majumba na kuweza kuwakamata baadhi yao waliohusika katika tukio la kumpiga na kumjeruhi dereva wa gari dogo aina ya escudo na kuwafikisha katika Kituo Cha Polisi.
















No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)