Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo.
Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya Azam FC wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.
SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.
Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao
Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog
Wawakilishi
wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, AZAM FC, wamerejea
jijini Dar es Salaam leo asubuhi na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki
na wapenzi wa timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere.
Azam
waliwasili kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways ambapo baadhi ya
wachezaji wakiwapo wanaoichezea Taifa Stars kubaki Nairobi isipokuwa
Mcha.
Azam
ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara
walikuwa Nchini Liberia kuchuana na timu ya Barrack Young Controllers
(BYC) ambapo Azam walishinda 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi
ya Pili ya michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman
Monrovia, Liberia.
Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)