Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa
akionyeshwa Mfumo wa Maji Taka na Meneja Mazingira Bw Dominick Mariki
wakati Waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Kiwanda cha Bia cha
Serengeti Browarizi cha Jijini Dar es Salaam ambacho Wananchi
wanakilalamikia kinawamwagia Maji Machafu katika Mtaa wa Chamwenyewe
Changmbe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Terezya Huvisa
akimsikiliza Operesheni Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Serengeti Shekhor
Mokosare, Waziri alifanya Ziara ya kukagua na kuangalia Uchafuzi wa
Mazingira Unaoyanywa na Kiwanda cha Bia cha Sereneti cha Jijini Dar es
Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya
Huvisa akimsikiliza Bi Mwaka Washokela kuhusu Malalamiko ya Umwangaji
wa Maji Machafu ya Kiwanda cha Bia cha Seregeti katika Mtaa wa
Chamwenyewe, Changmbe Jijini Dar es Salaam.Picha na Ali Meja
-
Wito umetolewa na Waziri wa Mazingira ofisi ya makamu
wa Rais Bibi Terezya Huvisa kwa wenye viwanda na Hoteli za kitalii kote
nchini kuzingatia usafi wa mazingira sababu mazingira ni uhai. Alitoa
rai hiyo wakati wa ziara yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kutembelea
baadhi ya viwanda na Hoteli za kitalii.
Viwanda alivyotembelea ni pamoja na Serengeti Brewerries
ambapo iligundulika kwamba maji ya taka ya kwenye kiwanda yanatiririshwa
kwenye mifereji ya nje ya kiwanda ambayo iko kwenye makazi ya watu .
Hivyo bas wanaathiri waanchi wanaozunguka eneo hilo kwa harufu kali
ya maji ya kiwandani. Waziri amewapa siku moja uongozi wa kiwanda hicho
kurekebisha mara moja matatizo waliyokutwa nayo la sivyo hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi ya kiwanda.
Kiwanda kingine alichotembelea Waziri ni kiwanda cha
kuchapisha maandishi kwenye fulana na vipeperushi ambacho kinaitwa
CI Group kilikutwa na makosa mabalimbali ikiwamo uchafu wa mazingira
ya kiwanda kwa ujumla, mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi wa kiwanda
ni machafu sana hivyo kupelekea afya zao kuwa hatarini.
Hata hivyo wamiliki wa kiwanda hicho walikimbia baada ya kumuona Waziri
na ujumbe wake wakiwasili. Bibi Huvisa ametoa agizo kwa watu wa NEMC
kwenda kukifunga kiwanda hicho mara moja.
Waziri Huvisa pia alitembelea hotel mbalimbali ikiwamo
Coco beach Hotel ambayo mazingira yake ni machafu na pia imejengwa kinyume
na sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ya kujenga mita sitini kutoka baharini.
Waziri aliagiza Hotel hiyo ifungwe . Hotel zingine ni Golden Tulip
na Sea Cliff zote ziko maeneo ya Oysterbay ambapo wameagizwa kuwasilisha
cheti cha mazingira kama hawana hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwamo
Hotel kufungwa.
Mwisho Waziri amewataka wenye Hotel kutilia mkazo
swala zima la kutibu maji.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)