Wabunifu mitindo Jackline Kibacha na Anna Lukindo wakisindikizwa na Mama Balozi Joyce Kallanghe na Mama Rose Kiondo
Nje ya Jumba la Somerset
Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha
Anna, Jack na Duane kutoka Jamaica
Anna Luks
Mama Rose Kiondo, Samson Soboye, Mama Joyce Kallaghe, Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha
Barabara ya The Strand copy
London Fashion Week 2013.Picha zote za Urban Pulse
Imeandikwa na Urban Pulse na Freddy Macha
Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na
urembo katika maonyesho ya kimataifa ya
London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames.
Maonyesho ya
London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28.
Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi
na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta
vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji
tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii Tanzania
ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na
LFW kushiriki kwenye mashindano ya kutafuta
vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha
na Christine Mhando ndio wasanii
waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya
kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
Katika kuunga
mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania, Ubalozi wetu
Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia
wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa
Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na
sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile
Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli
hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Mshindi wa tukio
alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa
mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo
na vichwa vya waandaaji,
wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya
kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali
ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa
Kitanzania. Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi
waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi
ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo
inasemekana ina thamani ya Pauni Billioni
10 ama
shilingi Trillion 25 za Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)