Rais Jakaya Kikwete jana amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Picha Zote na IKULU.
Rais Kikwete alitembelea daraja hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na daraja hilo na kuwataka walitumie vyema katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia ardhi yao kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.
Kikwete amewaambia wakazi hao kuwa wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama wawekezaji na kununua maelfu ya hekta za ardhi yao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)