RAIS Jakaya Kikwete ametoa rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa TANU/CCM na mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa Kanisa la KKKT- Dayosisi ya kati kutoka kwa wamisionari, mchungaji Thomas Musa(86). - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS Jakaya Kikwete ametoa rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa TANU/CCM na mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa Kanisa la KKKT- Dayosisi ya kati kutoka kwa wamisionari, mchungaji Thomas Musa(86).

  Wasira akisaini kitabu cha waombolezaji kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete
---
 RAIS Jakaya Kikwete ametoa rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa TANU/CCM na mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa Kanisa la KKKT- Dayosisi ya kati kutoka kwa wamisionari, mchungaji Thomas Musa(86). Marehemu Thomas Musa aliyezaliwa desemba 6,1927 wilayani Iramba alifariki ijumaa iliyopita na kuzikwa jumanne wiki hii, kijijini kwake Kinampanda, Iramba, mkoani Singida.

Katika salamu zilizotolewa jana jumatano jioni nyumbani kwa marehemu na waziri wa nchi ofisi ya Rais Stephen Wasira, Rais amesema amesikitishwa sana na kifo hicho kutokana na mchango wa marehemu kwa taifa, hasa elimu na afya katika uhai wake.

Rais alisema CCM na Serikali yake inaungana na familia ya mjane na mtoto wa marehemu Jaji Kipenka Musa anayesimamia familia hiyo, katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Katika rambirambi hiyo ambayo hakutaka itangazwe, Rais amesema ingawa mzee Musa amefariki, lakini matendo yake daima yataendelea kukumbukwa na kuenziwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages