Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima akimsalimia Mwezeshaji wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Asina Omari (kulia) kabla ya kufungua
mafunzo ya Jinsia awamu ya pili mjini Morogoro leo. Kushoto ni Kamishna
wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Pereira
aliwataka maafisa wa jeshi hilo wahakikishe msongamano ndani ya magereza
nchini unapungua.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima ili afungue mafunzo ya
jinsia kwa maafisa hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla
ya kufungua mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.
Maafisa Magereza wakimsikiliza
kwa makini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Pereira Ame
Silima (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa
mafunzo ya jinsia mjini Morogoro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima (wa katikati waliokaa) akiwa na Viongozi watendaji, maafisa
wa Jeshi la Magereza, wawezeshaji wa mafunzo ya Jinsia, na watumishi
raia wa jeshi hilo katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi mafunzo
hayo. PICHA ZOTE
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)