Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza na maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Malemi licha ya kulipongeza jeshi hilo kwa hatua nzuri ya kuwateua maafisa mbalimbali wanawake, alilitaka jeshi hilo kuongeza juhudi zaidi kwa kuwapa nafasi ya uongozi wanawake ambao wana uwezo na sifa ya kuongoza.
Maafisa Magereza wakiifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi alipokuwa anatoa hotuba ya kufunga mafunzo ya jinsia yaliyokuwa yanafanyika mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (wa pili kutoka kulia) akimpa zawadi askari wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, Beatrice Sabo kwa kuwasilisha vizuri mada ya jinsi na jinsia wakati wa mafunzo hayo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Anayefuata ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta. Kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Asina Omari.
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (Kulia), akipokea taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kutoka kwa Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta . Kushoto ni Dk Juma Malewa, Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI. WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)