TAARIA KWA UMMA
FEBRUARY 6, 2013
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight)
Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana
walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la
ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday
Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.
IBF imeamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia
kwa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika
na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na
kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo
kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard
Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.
Kama Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana
atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King, Bob Arum
na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya
kujitangaza kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati ya nchi
zinazotoa mabingwa wa dunia.
Kama Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu
historia ya ngumi nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne
duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na WBA.
Shiriksiho la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina
makao yake makuu ya kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
ndilo lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.
IBF/Africa inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao
pamoja na makampuni mbalimbali bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia
Shauri ufadhili wa kuweza kuligombea taji hili.
Mungu mbariki bondia Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Amen.
Imetolewa na:
UTAWALA
Shiriklisho la Ngumi la
Kimataifa Afrika (IBF/Africa)
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)