Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Atomiki Duniani - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Atomiki Duniani


Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Mhe. Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) alipofika kumtembelea  Wizarani leo.
Mhe. Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani  akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Shirika hilo kwa  Mhe. Membe.
Mhe. Membe (kushoto) na Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.), Waziri wa  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani, Mhe. Yukiya Amano (hayupo pichani)  wakati akizungumza nao leo.
Mhe. Juma Duni Haji (kulia), Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar,  Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati), Naibu Waziri wa Maji  na Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa Ushirikiano wa  Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani,
Mhe. Yukiya Amano (hayupo pichani).
Mhe. Yukiya Amano (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki  Duniani akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo  yao leo. Wengine katika picha ni Prof. Manase Selema (katikati),  Mkurugenzi wa Divisheni ya Ulaya ya Shirika hilo na Bw. Conleth Brady,  Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Yukiya Amano mara baada ya mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages