MH. LOWASSA AZUNGUMZIA VURUGU ZA BUSERERE,MKOANI GEITA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MH. LOWASSA AZUNGUMZIA VURUGU ZA BUSERERE,MKOANI GEITA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli, kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi.

ujumbe wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindikizawajumbe hao.
...........................Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa, amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani  kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka  kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa  amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana  na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba  viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya,  nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu  isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.

Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa
baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha  mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza  kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam  kwenye eneo hilo.


Ujumbe huo uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika  kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa  kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi  millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages