Meli ya kivita ya kupambana na uharamia ya urusi yatia nanga Dar es salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Meli ya kivita ya kupambana na uharamia ya urusi yatia nanga Dar es salaam


Meli ya kivita  ya kupambana na uharamia aina ya  Anti Submarine iitwayo  Marshal Shaposhnikov’,  ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi. Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia. Meli hiyo imewasilisiku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh  akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
Balozi Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchini pia.
Baada ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli.
Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa  kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.
Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages