MAMIA WAMUAGA MAREHEMU GRACE CHAO JIJINI DAR ES SALAAM LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAMIA WAMUAGA MAREHEMU GRACE CHAO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Hatimaye Ndugu Jamaa na Marafiki waishio Jijini Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wenzake na Marehemu Grace Mathew Chao leo wametoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Mpendwa wao Grace katika zoezi lililofanyika Katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam ambako mauti yalimkuta Februari 17, 2013. Grace Chao alizaliwa Desemba 13, 1985.

Mwili wa Grace ulisafirishwa kuelekea Mazimbu Mkoani Morogoro ili kuwapa fursa wana jamii ya Mazimbu na Mzumbe ambako marehemu alizaliwa na kuishi zoezi ambalo litafanyika kesho Jumatano kabla ya Msafara kuelekea Marangu kwa mazishi. Ungana na Father Kidevu Blog katika tukio hilo.
 Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kazi na masomo walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.
 Mama wa Marehemu Grace (kushoto) akiwa na mwana familia mwingine wakati wa zoezi hilo leo.






Ilikuwa ni majonzi sana katika tukio hili, kwa Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.
 Wafanyakazi wa CRDB Bank walifika kutoa heshima kwa Mwili wa Mfanyakazi mwenzao.
 Vijana wa Mzumbe Wengi sana walijitokeza kumuaga Grace katika safari yake hiyo ya Mwisho.
Marafiki na vijana wa Mzumbe wakimfariji kaka wa Marehemu Edwin Ndesamburo Chao (kulia) kufuatia msiba wa dada yake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages