Waziri
wa Habari, Vijana ,UtamaduninaMichezoDkt. Fenella Mukangara akifungua
mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini
Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia
weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli
mbalimbali zinazofanywa na serikali.
Maafisa
Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja
naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi
wa kikao kazi hicho mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba
Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao
kazi hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada
kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano
Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano
wa Serikali mjini Dodoma.
Afisa
Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Sarah Reuben
akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Mmiliki
na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka
Iringa Bw. Majjid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya
mitandao ya kijamii kwa mawasiliano serikalini mjini Dodoma.PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)