Baadhi ya abiria wa treni linalofanya safari za ndani ya jiji la dar al-maarufu kama treni la mwakyembe wakiwa nje ya mabehewa yao huku wakisubiri kichwa cha treni hilo kutengemaa tayari kwa kuendelea na safari yake kama kawaida kichwa hicho kimepata itilafu kwenye eneo la Tazara au Buguruni Azam likiwa linaelekea Kwenye Kituo Cha Stesheni ya Dar es Salaam. Siku ya Leo Treni ya Mwakyembe imepata msukosuko ambapo asubuhi treni hiyo iliweza kugongwa na gari aina ya Land Cruiser eneo la Tabata Mwananchi na Kupelekea Gari kuumia lakini hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika Ajali hiyo ya leo ila ilipelekea usumbufu kwa Abiria waliokuwa wakisubiria treni hilo kwenye mida ya asubuhi.Picha na Bakari Mustapha Wa Lukaza Blog
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)