Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala awa mwenyekiti mabalozi wa Afrika Ubeligiji - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala awa mwenyekiti mabalozi wa Afrika Ubeligiji

 Balozi Joel M Nheleko wa Swaziland nchini Ubeligiji, ambaye alikuwa Rais wa Mabalozi wa Afrika nchini Ubeligiji aliyemaliza muda wake, akimkabidhi Balozi wa Tanzania Dk. Diodorus Kamala mfuko wenye vitendea kazi kama ishara ya kumkabidhi Urais wa Mabalozi wa Afrika Ubeligiji jijini Brussels juzi.
 --
Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala ameteuliwa na mabalozi wa nchi za Africa wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo kuwa Mwenyekiti wao.
 
Balozi Kamala amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini Ubeligiji, Joel Nheleko aliyemaliza muda wake. Tanzania itashikilia kiti hicho kwa muda wa miezi sita hadi Julai 1, 2013.
 
“Nimefurahi kupewa heshima hii, na naamini nitaitumia fursa hii kufahamiana vizuri na mabalozi wenzangu na kuvutia fursa za kiuchumi kwa nchi yetu,” alisema Balozi Kamala.
 
Wakati huo huo, juzi mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa Tanganyika, walimchagua Balozi Kamala kuwa mwenyekiti wao.Nchi wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia.
 
Nchi hizi zimeunganisha nguvu kutafuta wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya Bonde la Ziwa Tanganyika, ambapo eneo la bonde hili lenye wakazi wastani wa milioni 40 wanalenga kuliendeleza kwa ajili ya kujenga miundombinu, kurahisisha usafiri na usafirishaji, kujenga reli mpya na kuendeleza utalii.
 
Chini ya mpango huu wanalenga pia kuboresha viwanja vya ndege vya nchi wanachama vya Mbala, Kalemie, Bujumbura, Kigoma na Kasanga kwa nia ya kurahisisha usafiri wa anga katika ukanda huu.
 
Dk. Kamala amekabidhiwa jukumu la kuratibu mpango huu na kwa pamoja watatafuta fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya mradi huu.
 
Mwisho…

H.E.Dr Diodorus Buberwa Kamala 
Ambassador Extraordinary and Plenipotentiary

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages