ALBINUS KUGOMBEA UBINGWA WA DUNIA WA IBF KWA VIJANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

ALBINUS KUGOMBEA UBINGWA WA DUNIA WA IBF KWA VIJANA

For Immediate Release Media Contact: Onesmo Ngowi
IBF/Africa Notes 13 Tel: (+255) 754- 360828

Bondia kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu wa nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF. Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25.
 Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Joseph Agbeko na Ike Quartey.
Albinus Felesianu
Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto
Mpambano huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 29 March chini ya kampuni ya Kinda Boxing promotions ya bwana Kinda Nangolo!
Hili litakuwa pambano la pili la ubingwa wa dunia kwa vijana baada ya bondia Ilunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) kumtwanga bondia Gogito Gorgiladze wa Georgia jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini jumamosi iliyopita.
ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages