AIRTEL YATANGAZA ZAWADI ZA MASHINDANO YA MPINGA CUP - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AIRTEL YATANGAZA ZAWADI ZA MASHINDANO YA MPINGA CUP

 Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza zawadi za washindi kwenye mashindano ya Mpinga Cup
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akionyesha moja ya jezi zitakazotumika katika michuano  ya mpinga cup itakayoanza leo jijini Dar es saalam chini ya udhamini wa Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
..............................
Kiongozi mkuu  maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.

Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo

Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1. Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet 

Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii. 

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages