Waziri wa Habari,
Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu
za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha
msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini
Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea
kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na
kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo
chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo
ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni
nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo
ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukangara amewataka ndugu,
jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba
na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa
wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo
alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni
pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ
Mwaka 2008 aliamua kuanza
kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two
Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye
aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo
alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase ,
Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010
na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini
India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango
mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na
kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha
kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku
filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha hali yake ilibadilika jambo
lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti
ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen
Imetolewa na:
Mkurugenzi
Idara ya Habari(MAELEZO).
Dar es Salaam.
2 Januari 2013
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)