Baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, Estaratus Mtemanyenza akitoa shukrani wakati wa kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mbunge huyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angella Kairuki.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika (Kulia), akiwa katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Regia Mtema.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi na Msemaji wa Regia Foundation, Olivia Sanare akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema. habari kwa hsiani ya http://francisdande.blogspot.com/
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, ametimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwake, ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alihudhuria maadhimisho hayo na kusema demokrasia ya kweli haigaiwi katika sahani ya dhahabu, bali kwa kuipigania.
Makamba alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa, wanaopaswa kupigania haki hiyo ni vijana ambao wanayo nafasi kubwa katika safari ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015.
Makamba alitoa kauli hiyo jana usiku katika hafla ya kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Regia, aliyefariki kwa ajali ya gari Januari 14, mwaka jana - hafla iliyofanyiola katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akitoa mada iliyohusu vijana na namna anavyomfahamu Regia, Makamba alisema kama vijana watatumika vizuri katika demokrasia, watakuwa chachu ya maendeleo na kwamba ujana peke yake si sifa ya kuwa kiongozi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)