
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala,Duwani Nyanda akizungumza
na viongozi wa Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki ambapo
polisi walizuia ibada kufanyika jana katika Kanisa la Moravian Ushirika
wa Tabata jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ingehatarisha amani kwa
waumini hao.Picha na Pamela Chilongola
--
Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na kuwapo kwa mgogoro ambao kwa
siku ya jana ungesababisha vurugu kutokana na upande mmoja wa uongozi
wa kanisa hilo kutaka kusimikwa kwa nguvu huku upande mwingine ukikataa.





Jamani ndugu zangu wa Moravian mmejiabisha, mgogoro gani huu wa mpaka kuvihusisha vyombo vya ulinzi na usalama?!!! Mungu went aliyewapa kazi HiI kwa uaminifu mmemuweka wapi?! Hebu angalia kanisa lenyewe hili lilivyo masikini, badala ya kulikomboa kanisa kutoka katika lindi la umasikini nyie mnaendekeza migogoro isiyo na tija! Mwaitebele hebu shughulikia mgogoro huu kiroho acha kuufanya uwe wa kidunia. Wakristo wengi waelewa wamebaki wanakushangaa kwa namna unavyoshughulikia suala hili, na mpaka kufanya wafikirie labda kuna masilahi unayopata!! Ogopa sana mtu anayetumia pesa yake kuendesha migogoro ya kanisa, Jiulize anafaidika na nini?! Kama ni baraka tu kwa nini basi asiwape pesa hizo masikini, watoto wa Mitanni na wahitaji wengine? Mungu irudishe Moravian ya zamani, ninachokiona sasa ni watu wamejivalisha magwanda ya Moravian lakini moyoni mwao wana dini wanayoijua wao.
ReplyDelete