TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
JANUARI 28,
2013
Rais wa
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi atakuwa msimamizi mkuu wa mapambano ya ubingwa
wa yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 8 na 30 March 2013.
Mapambano hayo
ni yale yanayowakutanisha mabondia Richard Commey akipambana na Mgana mwenzake
Bilal Mohammed wakigombea mkanda wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG)
katika uzito wa Lightweight. Mabondia wote
wawili wana rekodi zinazovutia, Commey ana makazi yake katika jiji la London
nchini Uingereza.
Mpambano wa
pili siku hiyo utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana Fredrick Lawson
akipambana na bondia machachari Isaac Sowah. Wote wanaishi nchini Ghana.
Mapambano yote
yatafanyika wakati bingwa wa dunia wa zamani wa IBF Joseph Agbeko atakapochuana na
bondia Luis Melendez wa Mexico kugombea ubingwa wa dunia wa IBO katika uzito wa
bantam.
Mpambano
mwingine ambao Ngowi atasimamia ni kati ya bondia Helen Joseph wa Nigeria na Fatuma
Zarika wa Kenya ambao watagombea mkanda wa IBF wa mabara wa wanawake. Helen
Joseph ni mkazi wa Ghana wakati Fatuma Zarika anaishi nchini Ujerumani.
Maofisa
wengine watakaomsaidia Ngowi katika mapambano hayo ni pamoja na: Refarii: Rodger Barnor, Jaji namba 1 ni Fred
Ghartey, Ghana, Jaji namba 2 ni Confidence Hiagbe
na jaji namba 3 ni May Mensah Akakpo, Ghana
Mapambano haya
ni kati ya mapambano 100 ambayo IBF imepania kuyafanya katika ukanda wa Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati mwaka huu 2013.
Imetolewa
na:
UTAWALA
International Boxing Federation Africa
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)