MWANAHARAKATI WA MICHEZO TANZANIA WILHELM GIDABUDAY AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWANAHARAKATI WA MICHEZO TANZANIA WILHELM GIDABUDAY AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI ARUSHA

Wadau wa Michezo nchini wakizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha;kutoka kushoto ni Gadiel Urio PR wa Shughuli hiyo, Rogath John Stephen(Mwanariadha wa kimataifa na Mtoto wa John Stephen Akhwari) , Bw. Wilhelm Gidabuday ambae ni mwanariadha na mwanaharakati wa Michezo Tanzania na Phaustin Baha Sule Mwana Riadha na Mshindi wa medali ya nusu marathon.

......
Mwanariadha wa zamani na maarufu katika kuitanganza Tanzania katika masikio na macho ya mashabiki wa riadha duniani, maarufu kama WILHELM GIDABIDAY, wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha.

Gidabiday amesema kuwa lengo kuu la press conference hii ni kuwaomba watanzania kujitolea/kuonyesha uzalendo katika harakati alizozianzisha sasa za kuanzisha uchangiaji wa kuanzishwa kituo maalumu cha michezo cha Taifa. Namnukuu maneno haya "progress is a slow process", "huwezi kushinda vita kama huna eneo la kutrain wanajeshi wako" akimaanisha
watanzania hatujachelewa kuanzisha kituo cha michezo cha taifa bali tunaweza kuanza sasa na tukafanikiwa, Pia maana ya pili ni hatutaweza kufanya vizuri katika michezo kimataifa bila ya kuwa na kituo maalum cha kufundishia wachezaji wetu.

Kwa stori zaidi tembelea www.wazalendo25.blogspot.com na pia kwa audio kuhusu alichoongea tembelea www.victormachota.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages