Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gongo la
Mboto Jerry Silaa (katikati) akizungumza na wakandarasi wanaoshughulikia
upanuzi wa barabara ya Nyerere kuanzia makutano ya uwanja wa ndege
kuelekea Gongo la Mboto ambapo amesema kwa ujumla barabara inatanuliwa
kutoka barabara mbili kuwa barabara tatu na kuchimbwa mitaro ya mvua ili
maji yaliyokuwa yakiharibu barabara yaweze kupata njia.Amesema
ukubwa wa kazi nzima ni kilomita 1.6 utakaogharimu shilingi bilioni 1.8
na kuwa mradi huo unasimamiwa na wakala wa barabara yaani TANROADS. Aidha
Mstahiki Meya ameitaka serikali ya kata kumsaidia mkandarasi kuondoa
wafanyabiashara ambao wapo maeneo ya barabara ili kazi iweze kufanyika
kwa wakati kwa kuwa kazi hii inatakiwa kuisha mwezi Mei mwaka huu. Kulia
ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko
na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce
Msenduki.
Pichani juu na chini ni Injinia Eliseus Mtenga (katikati) kutoka
TANROADS Dar akitoa maelezo mafupi kwa Mh. Mstahiki Meya wa Ilala juu ya
mradi wa upanuzi wa barabara ya kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga
Mombasa hadi njia panda ya Kiltex na marekebisho ya eneo korofi karibu
na Sekondari ya Pugu ambapo amesema lengo ni kupanua barabara kwa Mita
3.0 kila upande ili kuwezesha njia tatu za magari kupatikana.
Hii
ni awamu ya tatu katika upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi
tatu ambapo awamu ya kwanza ilihusisha Kilometa 1.8 na Awamu ya pili
Kilometa 2.5 zilishakamilika. Kushoto ni Injinia Eliamin Tenga wa
TANROADS na kulia ni Site Engeneer wa mradi huo Godson Tenga.
Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto) akiongozana na Wakandarasi
wa TANROADS pamoja na viongozi wa Kata ya Gongo la Mboto kukagua mradi
wa barabara hiyo.
Injinia Eliseus Mtenga (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Mstahiki Meya.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akiendelea na ukaguzi wa barabara ya kuelekea Gongo la
Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi njia panda ya Kiltex yenye urefu wa
Kilometa 1.6.
Pichani
Juu na Chini ni Muonekano wa Barabara ya Kuelekea Gongo la Mboto
kuanzia Ukonga Mombasa hadi Njia Panda ya Kiltex ikiwa kwenye
matengenezo ya kuweka mifereji ya kupitisha maji ambayo yamekuwa
yakiathiri barabara kipindi cha Mvua.
Injinia Eliseus Mtenga akiendelea kutoa maelezo ya mradi huo kwa
Mstahiki Meya Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la
Mboto.
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika barabara hiyo kama inavyoonekana pichani.
Pichani
Juu ni Msongamano wa magari na wapita kwa miguu kutokana na
ufinyu wa barabara unaosababishwa na usafiri wa daladala pamoja na
wafanyabiashara waliopanga bidhaa zao kando kando mwa barabara hiyo
ambao wanatakiwa kuondoka mara moja ili kupisha upanuzi wa barabara
hiyo.Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)