Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akihutubia kwenye uzinduzi wa Chanzo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhandisi Evaristi Ndikilo akimwekea chanjo mmoja ya kati ya watoto
walioshiriki kwenye Uzindu wa Chanjo kwa Mtoto 13 Mkoani Mwanza
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akishiriki kwenye buradani
ya msanii mchelemchele muda mfupi baada ya Kuzindua Chanjo kwa Mtoto
2013 Mkoani Mwanza Leo
---
Zoezi la Chanjo limefanyika kimkoa katika Wilaya
ya Sengerema kwenye Tarafa ya Sengerema kijiji cha Sima na Kata ya Sima Mkoani Mwanza.
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo
amesema zoezi hilo kimkoa ni lazima lifanikiwe kwa mujibu wa malengo
walio jiwekea ya 95% kwa kila wilaya kinyume chake wale wote watakaoshindwa
kufikia lengo itabidi wajieleze na sababu zilizofanya washindwe kuvuka
malengo katika Mkoa wake.
Ndikilo amesema yeye kama mtendaji Mkuu katika Mkoa wa wa Mwanza hayupo
tayari kuona Mkoa huo unakuwa wa mwisho katika zoezi hilo.
Amewahimiza wazazi kujitokeza kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo
hiyo kwani kuacha kuwachanja watoto, si hatari kwa mototo tu, bali pia
watoto wenzake wanao mzunguka hivyo ni vema kila mzazi akaona umuhimu
wakumpeleka watoto katika chanjo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa Sengerema na Mkoa wa
Mwanza kwa ujumla wake kuwa, chanjo hiyo ni salama kwakuwa imefanyiwa
utafiti wakutosha na wataalam wa afya wa Ulimwenguni na Wizara
ya afya hapa nchini.
Akihututubia mamia ya wananchi wa kijiji hicho cha Sima, Amesema
watoto wa chini ya miaka 5 wanachangamoto nyingi, hasa kwenye nchi zetu
hizi zinazo endelea , kwani kwingineko kwa nchi zilizo endelea watoto
wanao zaliwa hukua kwa takriba ni 99% tofauti na hapa kwetu.
Amesema ugonjwa wa kichomi huua watoto kwa 14% ukitanguliwa na Malaria
ambao huuwa kwa asilimia 15% huku ugonjwa wa kuharisha ukishika nafasi
ya tatu kwa kuuwa watoto wengi kwa asilimia 12% kwani nchini Tanzania
kila mwaka watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao takriba
ni 198,443 huugua ugonjwa wa kuharisha na kati yao 13,397 hufariki dunia.
Ujumbe mahususi wa siku hiyo ni Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye
afya, ameongeza kuwa Chanjo hiyo ni sehemu ya Ilani, hivyo kufika 2015
jamii ya kitanzania iwe ni jamii iliyo na ustawi.
Magonjwa ambayo hadi hivi sasa yana chanjo ni donda koo, kichomi,
kuharisha, pepopunda, kifua kikuu, surua, homa ya uti wa mgongo, kifaduro,
homa ya ini, na polio, haya ndio magonjwa yaliopo katika mpango wa
Taifa wa chanjo alisema na kuongweza.
Amehiza viongozi wa kila ngazi kuzindua kampeni hiyo,
na watoto walengwa ambao ni kuanzia wiki 6 hadi wiki 32 wapatiwe chanjo
hiyo bila kukosa.
Jumla ya watoto 149,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hiyo na amesema
zoezi hilo ni endelevu hadi tarehe 31. DEC. 2013.
Kaulimbiu ya katika maadhimisho hayo ni kuwa “Mtoto asiye chanjwa ni hatari
kwake na kwawenzake, mpeleke mototo wako akachanjwe”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)