Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja (katikati) akikagua gwaride la heshima la wahitimu wa mafunzo
ya awali ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi
namba 7 katika Chuo cha Udereva na Ufundi cha jeshi hilo (KPF) kilichopo
Kingolwira nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akimpongeza Beatrice Dugange baada ya kumpa cheti na leseni
ya udereva baada ya kumaliza mafunzo ya udereva chuoni hapo. Jumla ya
wanafunzi 66 walipatiwa vyeti na leseni kwa kuhitimu mafunzo hayo.
Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake na baadaye kufunga mafunzo hayo
ya awali.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkono wa Mara iliyopo
chuoni hapo wakitumbuiza katika sherehe hiyo kwa kutoa michezo mbalimbali
mbele ya mgeni rasmi, Kamishna Jenerali John Minja.
Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza kwa makini, Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja wakati akitoa
hotuba yake na baadaye kuyafunga mafunzo ya udereva wa magari kozi
namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7. PICHA ZOTE
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)