Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya
Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao
waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi
na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka
kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua
wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa
linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu,
wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya
ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao,
wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya
ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa
mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita
kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza.
Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa kike wakiwa katika mahafali hayo leo.
Baadhi ya wahitimu wa kiume, wakiwa katika mahafali hayo leo.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Khadija Hassan,
wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya
ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Dua baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Mama
Asha, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wanafunzi
wahitimu wa kidato cha sita, baada ya zoezi la kugawa vyeti kwa
wahitimu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)