Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi. Maria Kashonda.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta (katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro Mohammed (kulia) mara baada kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (jumatatu januari 21, 2013) jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju na Wajumbe wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo
Kamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi maoni ya LRCT hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohammed.
Mjumbe wa Mtandao wa Kinga Jamii (TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi. Clotilda Isdor akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko uliofanyika leo (jumatatu janauari, 21, 2013). Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)