Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki akiogea na viongozi wa PPF Pensheni Fund wakati walipotembelea TSN kufahamiana na kujifunza mambo mbalimbali katika makutano ya barabara za Nelson Mandela na Nyerere Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw.Steven Alfred,Meneja wa Kanda, Mbaruku Magawa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Msanifu kurasa wa gazeti la HabariLeo, Ephraim Mwaluvinga (kulia) akiwaonesha jinsi maadalizi ya gazeti yanavyofanywa kwa ugeni kutoka PPF ulipotembelea chumba habari cha gazeti hilo Dar es Salaam jana.
Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
Fundi Mitambo wa TSN, Rashid Singandole, akieleza jinsi mitambo ya uchapaji ya Standard Printers inayomilikiwa na TSN inavyofanya kazi, kwa uongozi wa PPF uliotembelea kiwanda hicho. Kuanzia kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji,Steven Alfred, na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo,Bi. Lulu Mengele.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akiueleza jambo ugeni wa PPF baada ya kutembelea mitambo ya kampuni hiyo muda mchache kabla ya kuondoka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)