MAREHEMU LIDYA LEO ALIYEUAWA CHUO CHA MTAKATIFU JOHN KAMPASI YA DODOMA AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO MATOMBO MKOANI MOROGORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAREHEMU LIDYA LEO ALIYEUAWA CHUO CHA MTAKATIFU JOHN KAMPASI YA DODOMA AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO MATOMBO MKOANI MOROGORO

 Habari Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Marehemu Lidya Leo mwenye umri wa miaka 57 na Mzaliwa wa Matombo Mkoani Dodoma aliyeuliwa siku ya jumapili  majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa Chuo Cha Mtakatifu John Dodoma alipokuwa akirejea kutoka Kwenye Masomo ya Jioni kwenda Nyumbani kwake amezikwa Leo Kijijini Kwao Matombo Mkoani Morogoro. 
 
Marehemu Lidya Leo ambae alikua ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 aliyekuwa anasoma shahada ya Kwanza ya Unesi ya Chuo Kikuu Cha Mtakatifu John Kampasi ya Dodoma Aliuliwa  Mnamo Jumapili majira ya saa nne usiku na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na hatimaye kutelekeza mwili wakena kupelekea Mwili wake kuharibiwa vibaya na mnyama ambaye mpaka sasa hajajulikana kwa kunyofolewa macho, masikio, pua, mguu na baadhi ya viungo vingine katika mwili wake.
 
Mwili wa Marehemu Lidya Leo umefikishwa Leo kijijini Kwao Matombo Mkoani Morogoro ukitokea Mkoani Dodoma Ambapo ndio alikua akiishi kutokana na kuwa alikua masomo mkoani hadi mauti Kumfika.
 
Marehemu amezikwa Leo Jumanne Kwenye Majira ya Saa tatu kasoro usiku Kijijini kwao Matombo Mkoani Morogoro na mazishi hayo kuhudhuriwa na Wanafunzi takribani 170 kutoka Chuo Cha Mtakatifu John ambapo marehemu alikua ni Mwanafunzi wa Chuo Hiko Mpaka Mauti yalipomfika.
 
Akiongea Kwa Simu na Mmiliki wa Mtandao huu wa Lukaza Blog Bw Joachim Leo ambaye alikua akimuita marehemu Mama Mdogo amesema Kuwa Analiomba Jeshi la Polisi Kuweza kufanya Uchunguzi na Kuhakikisha linawakamata wahusika wote waliohusika Katika Mauaji haya ya Kinyama ya Marehemu Lidya Leo na Kufikishwa Kwenye Vyombo Vya Sheria.

Marehemu Lidya Leo ameacha Mtoto mmoja.

Lukaza Blog Inatoa Pole Kwa Familia ya Bwana na Bibi Leo na Kuwaombea Mungu awape Nguvu na Ujasiri Katika Kipindi Hiki Kigumu Cha Msiba wa Mpendwa Wao Marehemu Lidya Leo ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa Chuo Cha Mtakatifu John Kampasi ya Dodoma.

Vilevile Lukaza Blog inatoa Pole Kwa wanafunzi wa Chuo Cha Mtakatifu John, Uongozi wa Chuo Hiko Pamoja na Ndugu jamaa na Marafiki wa Marehemu Lidya Leo Kwa Kuondokewa na Ndugu yao Kipenzi.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages