Manispaa ya Kinondoni imekabidhiwa
vifaa 100 vya kutunzia taka na benki ya BankABC vyenye thamani ya
shilingi milioni 3.5 leo Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda
amesema Manispaa yake itahakikisha usafi unazingatiwa na mkazi
atakayebainika kutupa taka ovyo atachukuliwa hatua kali ikiwemo kumtoza
faini ya kuanzia shilingi 50,000 mpaka 10,000
“Hii ni kampeni maalumu
tuliyoizindua ya kuweka safi Mazingira ya Manispaa yetu. Sasa natoa wito
kwa wakazi wa Manispaa kuvitunza vifaa hivi sambamba na kuyatunza
mazingira vinginevyo haitasita kuwatoza faini. Na faini yetu itaanzia
shilingi 50,000 hadi shilingi 10,000.” Alisema. Naye Ofisa Masoko wa benki hiyo,
Evelyn Auguste amesema wameamua kushirikiana na Meya huyo baada ya
kuvutiwa na kampeni hiyo ya utunzaji wa Mazingira.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)