Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Kimataifa la afya ya uzazi jijini Arusha leo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Kimataifa la afya ya uzazi jijini Arusha leo



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akizungumza wakato akifunga kongamano la Kimataifa la Afya ya Uzazi la siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Pichani toka kulia ni Naibu Wazirii wa Afya,Dkt. Seif Rashid (Kulia) ,Waziri wa Afya Zanzibar,Dkt. Juma Haji Duni (kati) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo wakifuatilia Kongamano hilo.
Baadhi ya wataalamu wa kongamano la Kimataifa la afya ya uzazi wakimsikiliza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano hilo leo jijini Arusha, ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani na nje ya nchi wamehudhuria.
Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar,Dkt. Juma Haji Duni akiongea katika kongamano hilo leo mjini Arusha.kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo
Mke wa Rais na Mwenyikiti wa Taasisis ya WAMA ,Mama salma Kikwete (alievaa kitenge) akiogozana na watendaji wakuu wakielekea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo.
Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha.
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Kimataifa la Afya ya Uzazi.Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages