Mtaalamu
wa kubuni Ofa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya TIGO Jacqueline
Nnunduma akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena Dar
es salaam leo jijini Dar es salaam kuielezea ofa hiyo.
……………………………………………..
Tigo imetambulisha huduma mpya kwa
wateja ujulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la
gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana
na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.
Kusajili huduma kwa mteja piga
*149*90# au tuma neno “TIGO TIME” kwenda namba “15372” na baada ya hapo
utapokea ujumbe ambao utaonyesha kwamba umefanikiwa kusajili na unaweza
kuanza kutumia huduma hii na ufurahie punguzo kubwa sana la gharama.
Baada ya kusajili, Tigo Time itakujulisha punguzo lako la gharama la
kupiga simu kutokana na muda wa siku na eneo ulipo. Gharama ya huduma
hii ya kusajili itakuwa ni Tshs 149 kwa kiwango cha chini.
“Tigo inatambua kwamba wateja wetu
wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu na hii ni njia mojawapo ya
kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa juu na
vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda wowote.” Alisema
Bi. Jacqueline Nnunduma, Mbunifu wa ofa za Tigo. “Kwa punguzo hili kubwa
la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo Time itakuwa huduma
maarufu kama ilivyokuwa huduma ya ya Kwa Sekunde tuliyoianzisha miaka
kadhaa iliyopita.” Alimalizia Bi. Nnunduma.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu
za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana
katika mikoa ishirini na sita (26) Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao
unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja
wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za
bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za
fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya Millicom International Cellular S.A (MIC) ambayo
ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja
milioni 43 katika masoko 13 barani Afrika na Amerika ya Kusini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)