IGP SAID MWEMA AKABIDHI PIKIPIKI 564 KWA POLISI NCHI NZIMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

IGP SAID MWEMA AKABIDHI PIKIPIKI 564 KWA POLISI NCHI NZIMA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kovaakijaribhu mkuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nch nzima mara baada ya makabidhiano anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba
Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages