Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alifanya ziara ya ghafla kulikagua jengo la mikutano la Chachani Chake Chake Pemba, hapa alikuwa akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Canal Mstaafu Juma Kassim Tindwa, jinsi ya kulinusuru jengo hilo.
Jukwaa la ukumbi wa Mikutano wa Chachani chake, lililokuwa likitumiwa na waheshimiwa kwa mikutano na Vikao sambamba na burudani, ambalo kwa sasa limekuwa makazi ya mchwa.
Hii
ni hali halisi ya eneo la ndani ya ukumbi maarufu wa mikutano uliopo
Chachani Chake Chake Pemba, ambao awali ukumbi huo ulikuwa ni jengo
maalum la sinema.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea kukagua
kwa nje ya jengo la ukumbi wa mikutano la Chachani Chake Chake Pemba,
ambalo liko katika hali mbaya.Mpiga picha Hassan Issa- OMPR-ZNZ
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)