Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bw Sam Elanagaloor akielezea huduma ya 'One network' kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)ambapo leo airtel imezidua huduma itakayowaweze wateja wa airtel wanaosafiri kwenda India, Srilanka na Bangladesh kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na watafaidi kupokea simu bila malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi wakiwa katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza mwaka, biashara au matibabu (leo) katika ofisi kuu ya Airtel Tanzania
=============== ============ ============
Airtel yaleta kingine cha kwanza kupokea simu bila gharama yoyote India
* Wateja wa Airtel kupokea simu bure wakiwa nchini India
* Huduma hii pia itapatikana Srilanka and Bangladesh
Jumatano 12 Desemba 2012, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika msimu huu wa sikukuu imewawezesha wateja wote nchini kuendelea kutumia laini zao za Airtel Tanzania wakiwa India na kufurahia kupokea simu bila makato yeyote na kuwahakikishia uhuru wa kuongea wakati wa msimu huu wa sikukuu.
Akitoa ufafanuzi juu ya huduma hii ijulikanayo kama "One Network Asia" Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw Sam Elanagaloor alisema" wateja wetu kutoka Tanzania wanaosafiri kwenda India, Srilanka na Bangladesh wataweza kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na watafaidi kupokea simu bila malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi wakiwa katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza mwaka au biashara
"Tunafahamu kuna watanzania wengi wanapata matibabu nchini India, kuna watanzania wengi wanasoma nchini India, Tunaamini kwa kupitia huduma hii tutawawezesha watanzania wengi wanaotembelea na wale wenye ndugu nchini India kuwasiliana bila gharama yeyote sio tu katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ila na siku za usoni. Mteja anachotakiwa kufanya ni kuongeza muda wa maongezi kwenye laini yake ya Airtel Tanzania na kufurahia huduma za Airtel" aliongeza Elangalloor.
Mbali na kuzinduliwa kwa huduma hii inayota unafuu kwa wateja wa Airtel watakaofanya safari zao kwenda India Srilanka na Bangladesh, wateja wa Airtel wote pia wataendelea kufurahia huduma huduma ya 'One network' (kutumia laini zao za nyumbani) katika nchi 17 za Afrika ikiwemo: Kenya, Uganda, Malawi, DRC, CongoB, Madagascar, Nigeria, Ghana, Rwanda, Zambia, Niger, Gabon, Burkina, Sierra L,Chad, Tanzania.
"Hili ni la uhakika kabisa kwa kuwa mtandao wetu ni mpana, wateja wa Airtel wanaposafiri kwenye nchi hizo wanaunganishwa na kupiga simu kwa bei nafuu, kuongeza salio kwa kutumia vocha za nchi walizotoka wakiwa popote, pamoja na kuunganishwa na huduma ya internet" alimaliza kwa kusema Elangalloor
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)