Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib Bilal (kushoto) alipowasili jana katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza akipokewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataia Mhe. Bernard Membe
Rais Joseph Kabila wa DRC akipokewa na Waziri wa Uvuvi Dr, David Mathayo.
Makamu wa Rais wa Zambia Dr. Guy Scott akifurahia jambo na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe aliyempokea
Balozi wetu nchini Msumbiji Shamim Nyanduga (kulia) akiongea na baadhi ya maafisa wa SADC
Kikundi cha matarumbeta cha Mount Usambara kinachoongozwa na Mzee Hoza kikitumbuiza uwanjani
Bendera za nchi zinazojumuisha nchi za SADC zikipepea. Picha zote na Manakombo Jumaa-MAELEZO

Viongozi
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika,
SADC, wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini
Tanzania. Kikao
cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA
kilianza jana Ikulu jijini Dar es salaaam chini ya Mwenyekiti wake Rais
Jakaya Kikwete.
Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Amesema mara baada ya kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa sasa SADC.
Viongozi hao kwa pamoja watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi wote 14 wa SADC utakaofanyika leo jijini Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)