Afisa habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma akitoa maelezo ya awali kuhusiana na mafunzo hayo yanayolenga kuwawezesha vijana kuwa na uelewa na mbinu juu ya ujasiriamali na namna ya kusimamia biashara zao ili kuongeza uzalishaji hivyo kupambana na kuupunguza umasikini katika ngazi zao kabla ya kumkaribisha Mratibu wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana Bw. Louis Mkuku (kushoto).
Mratibu
wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana Bw. Louis Mkuku
akifungua rasmi mafunzo hayo ambapo ametoa hamasa kwa vijana kutumia
vizuri elimu watakayoipata wakati huu wa ujana wao kujenga maisha ya
baadae na kuahidi kufuatilia kwa umakini matokeo ya mafunzo hayo na
kusema atahakikisha kila mwenye ndoto itatimia kwa usimamizi wa ILO na
UNIC.
Ameongeza kuwa pamoja na kupata uelewa juu ya ujasiriamali mafunzo hayo yanakwenda sambamba na lengo namba 1 la Maendeleo ya Milenia ambalo ni Kupunguza Umasikini, kwa kuwa yatawapatia mbinu zitakazowawezesha kuboresha shughuli zao za kujipatia kipato hivyo kuwa na kipato endelevu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)