Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) na Naibu wake
Mh. Angellah Kairuki (kulia).
Sasa
imezinduliwa rasmi....Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa
wageni waalikwa (hawapo pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu)
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri
Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias
Chikawe (kushoto).
Waziri Mkuu Pinda akipitia ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini
(UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kikundi
cha Wana wandime ya kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Pichani
Juu na Chini ni Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo
za serikali, Wanafunzi wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu
na Wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Waziri wa Katiba na Sheria na
Naibu wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja
baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu huku
akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mgeni
rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na
kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot.
Pichani
Juu na Chini ni maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu
yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali,
Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu
yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri
mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)