Mwenyekiti
wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania
Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa
Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata ambaye ni Muanzilishi wa
taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata
Foundation,wakati wa kuadhimisha Miaka Mitano ya Onyesho la Mavazi la
Tanzania Red Ribbon Fashion Gala ambalo hufanyika Desemba 1,kila mwaka
ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika kwenye Hoteli
ya Serena,jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania
Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabithi Cheti kwa
Dada Halima Rashid.
Mwenyekiti
wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania
Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa
Mkurugenzi wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Beccon.
Wanamitindo wakipita jukwaani kuonyesha mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Wabunifu wa hapa nchini.
Waendeshaji
wa Onyesho hilo,Evans Bukuku (picha ya juu) na Abby wakionyesha nao
umahiri wao wa kutembea jukwaani kwa mwendo wa kiuana Mitindo.
Mwanamitindo
Maarufu nchini,Flaviana Matata (kushoto) ambaye ni Muanzilishi wa
taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo ya Flaviana Matata
Foundation akiongoza mnada wa nguo walizozivaa kwa ajili ya kukusanya
hela ya kusaidia wahitaji walio chini ya Taasisi hiyo,ambapo hadi mnada
wa vitu mbali mbali unamalizika jumla ya shilingi Milioni 72 ziliweza
kukusanywa hiyo jana.Kulia ni Mwanamitindo,Jenuffer Bash.
Wadau wakifatilia kwa Umakini Onyesho hilo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)