SWAHILI FASHION WEEK 2012 YAHITIMISHWA MWISHONI MWA WIKI HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SWAHILI FASHION WEEK 2012 YAHITIMISHWA MWISHONI MWA WIKI HII


Gabriel mollel receiving the DESIGNER OF THE YEAR award from Hon. jerry Silaa.
Ailinda Sawe receiving awards from Dana Banks director of pUBLIC Communication at US emnbassy in Dar es salaam.
--
*GABRIEL MOLLEL ANYAKUA TUZO MBILI
*GABRIEL KUIWAKILI SWAHILI FASHION WEEK KATIKA MAONYESHO YA MITINDO MSUMBIJI 2012
 
Baada ya miezi mingi ya maandalizi, waandaji wa Swahili Fashion Week wamefanikia kuhitimisha onyesho kubwa la mitindo na mavazi katika nchi za Afrika mashariki na kati, tukio lilinaloendelea kuiweka tasnia ya mitindo katika ramani ya mitindo Afrika na Duniani kiujumla.
 
Ikiwa na viwango vipya na vyenye ubora, waandaji wamefanikiwa kuwa na tukio bora la mwaka na kuwaacha wahudhuriaji wakihitaji maelezo zaidi kuhusu onyesho la 2013. Kama ilivyo ada vitu vizuri lazima viwe na mwisho, Swahili Fashion Week 2012 ilimalizika kwa kutolewa tuzo siku ya Jumamosi ya tarehe 8, Desemba 2012.
 
Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zimelenga kutambua mchango wa wabunifu mbalimbali ambao wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia ya mitindo Afrika Mashariki. Tuzo hizo zinaongeza chachu ya uvumbuzi na ubunifu katika tasnia ya mitindo. Hii inaendana na kuifanya mitindo ya Kiswahili kujulikana duniani. Alisema Mustafa Hassanali, Mmiliki na Muandaaji wa Swahili Fashion Week.
 
Swahili Fashion Week 2012, imefanyika katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 6-8 Desemba, ikiwa tukio kubwa la Mitindo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati lililokutanisha wabunifu zaidi ya 50 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
 
Mshindi wa Tuzo mbili mwaka huu, Mbunifu Mvumbuzi wa mwaka na Mbunifu Bora wa Mwaka, Gabriel Mollel ataiwakilisha Swahili Fashion Week katika week ya mitindo Msumbiji inayoanza Desemba 7-15. Kwa mwaka wa tano sasa Swahili Fashion Week imefanikiwa kuendeleza uhusiano na Mozambique Fashion Week.
 
“Ni faraja kuiwakilisha Tanzana na Swahili Fashion Week katika maonyesho ya Msumbiji, kushinda tuzo mbili mwaka huu, kwangu ni matokeo ya kujituma na ubunifu mzuri, ninatumia muda mwingi kutengeneza kazi zangu. Hii tuzo inanipa nguvu kubwa lakini ni changamoto kwani kazi ngumu katika maisha ni kubaki katika hadhi ile ile ambayo watu walikuamini na kukupa katika shughuli unayoifanya”Alisema Gabriel
 
“Kama Swahili Fashion Week ni jambo la fahari na kujivunia kuwa sehemu ya Mozambique Fashion Week, Gabriel Mollel hataiwakilisha tu Swahili Fashion Week nchini Msumbiji, ila pia anaiwakilisha nchi yetu kwa kuonyesha ubunifu na mitindo iliyotengenezwa Tanzania” Alisema Mustafa Hassanali.
 
Huu ni mwaka wa Tano sasa tangu Swahili Fashion Week ianze kushirikiana na Mozambique Fashion Week ambapo Mustafa Hassanali alishiriki mwaka 2007 na 2008 huku Jamila Vera Swai akiwakilisha 2009, Manju Msita 2010, Robbi Morro na Ailinda Sawe wote walienda 2011.
 
“Swahili Fashion Week inalengo la kutangaza, kuinua na kutafuta masoko ya bidhaa za wabunifu wa Afrika Mashariki katika soko la Afrika na duniani kote. Tasnia ya Mitindo afrika inaitaji kutambiliwa na kuwekwa katika ramani ya dunia” Aliongeza Mustafa Hassanali.
 
Licha ya kutambua mchango wa wadau mbalimbali wa tasnia ya mitindo Afrika Mashariki, SFW pia ilitoa nafasi kwa wabunifu vijana wanaochipukia kuonyesha kazi zao na mitindo yao kwa mashabiki wa mitindo waliohudhuria katika Swahili Fashion Week mwaka huu ambapo wabunifu mbalimbali walionyesha ubunifu wao.
 
Wabunifu wa Swahili Fashion Week pia walipata nafasi ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na USAID COMPETE kwa kushirikiana na ORIGIN AFRIKA juu ya kutafuta masoko kwa bidhaa wanazozitengeza.
 
Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Taifa),Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax, Natol na 361 Degrees.
--

FEMALE MODEL OF THE YEAR - Nadia Ali
MALE MODEL OF THE YEAR - Benson Kwembe

EAST AFRICAN MODEL OF THE YEAR - Joseph Kimeu (KE)

DESIGNER OF THE YEAR - Gabriel Mollel

EAST AFRICAN DESIGNER OF THE YEAR - John Kaveke (KE)
MENSWEAR DESIGNER OF THE YEAR - Martin Kadinda

UPCOMING DESIGNER OF THE YEAR - Lucky Creations

INNOVATIVE DESIGNER OF THE YEAR - Gabriel Mollel

REDDS FEMALE STYLISH PERSONALITY - Nancy Sumari

MALE STYLISH PERSONALITY - Andrew Mahiga

VODACOM FASHION BLOG OF THE YEAR - Missie Popular

FASHION PHOTOGRAPHER OF THE YEAR - Osse Greca Senare

FASHION JOURNALIST OF THE YEAR - Maimuna Kubegeya (MCL)

EAST AFRICAN JOURNALIST OF THE YEAR - Susan Wong (Capital Group)

FASHION TV PROGRAMME OF THE YEAR - Nirvana (EATV)

Best Exhibition Stand – Codesh Jewellery

Origin Africa Award – Ailinda Sawe

New Face of the Year – Rachida Usuale

Emerging designer Competition Award – Phylista Oniango – Kenya

Humanitarian Award – Asia Idarous

Zakhia Meghji Lifetime Achievement Award – Farouque Abdela – Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages