VIONGOZI
WA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) WAKIWA KATIKA MKUTANO WA
MAANDALIZI YA FAINALI ZA TAIFA ZA MISS UTALII TANZANIA NA BODI YA
MISS UTALII TANZANIA 2012/2013 ZITAKAZO FANYIKA HIVI KARIBUNI.
WAJUMBE
WA BODI YA MISS UTALII TANZANIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA
VIONGOZI WA BARAZA LA SANAA TAIFA (BASATA) BAADA YA KIKAO CHA MAANDALIZI
YA FAINALI HIZO ZA MISS UTALII 2012/2013.
************************************************
Wakati
kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/2013 ikikaribia kuanza katika Hotel
ya Ikondolelo Jijini Dar es salaam, juzi tarehe 14.12.2012 Bodi ya Taifa
ya mashindano hayo ilifanya kikao na Serikari kupitia Baraza la Sanaa
la Taifa katika ukumbi wa Baraza hilo. Katika kikao hicho ambacho
kilijadili maandalizi ya fainali na mpango mkakati wa fainali za taifa
za Miss Utalii Tanzania mwaka huu.
Katika
kikao hicho Bodi ya Miss Utalii Tanzania iliwasilisha taarifa ya
kukamilika kwa maandalizi kwa Serikali ambapo bodi iliitaarifu Serikali
kuwa maandalizi ya fainali hizo yamekamilika kwa asilimia tisini 90%
ikiwemo katika maeneo ya kambi na mafunzo, ukumbi, Zawadi,
wadhamini,Washiriki, Nk.
Bodi
ilibainisha kuwa kwamba jumla ya washiriki sitini (60) wakiwakilisha
mikoa yote ya Tanzania na Kanda maalum za vyuo vikuu watapanda jukwaani
kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/2013. Pia Bodi ilibainisha
kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa washindi zimelenga zaidi kuwanufaisha
washiriki , jamii zao na taifa. Zawadi hizo ni pamoja na Nafasi za
masomo za elimu ya juu, mikataba ya kazi ,Safari za kushiriki mashindano
ya Dunia na Kimataifa , Tuzo za heshima za kijamii, kitalii,
kitamaduni, urembo na mitindo.
Aidha
Bodi ilielezea kuwa imejipanga kuzifanya fainali za Taifa za Miss
Utalii Tanzania 2012/2013 kuwa tukio kubwa la pekee Kihistoria na
kitamaduni kuwahi kufanyika nchini kabla na baada ya uhuru. Ambapo
wakiwa kambini washiriki watafanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja
na kupata mafunzo stadi mbalimbali za maisha , uhamasishaji na
utangazaji wa elimu , utalii, utamaduni, uwekezaji,mazingira, michezo na
afya.
Nayo
Serikali ilipongeza Bodi ya maandilizi ya miss utalii Tanzania kwa
mpango mkakati na maandalizi yenye kukidhi na kulenga kupromoti
utalii uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utamaduni,
uwekezaji,mazingira, michezo na afya.Akizungumza katika mkutano huo
Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifda Ndugu.
Malimi
Mashili alipongeza mpangilio wa zawadi na tuzo kwa washindi pamoja na
washiriki ambapo tofauti na mashindano mengine ambapo zawadi zao huwa ni
mzigo kwa washiriki na wakati mwingine zisizo na manufaa kwa jamii wala
Taifa."Miss utalii Tanzania katika kipindi cha miaka mitano tangu
kuanzishwa kwake imekuwa ni fahari ya Taifa na kielelezo cha utamaduni
wa Tanzania kitaifa na kimafaifa ambapo limekuwa ndilo shindano pekee
linalo la tangaza nchi yetu kwa kushinda mataji ya Dunia na kimataifa
kila mnapo shiriki".
Aidha
akiahirisha mkutano huo aliihakikishia Bodi kuwa Serikali inatambua
juhudi na mchango wa waandaaji na mashindano ya miss utalii tanzania
katika kukuza utalii, utamaduni na michezo nchini na kwamba Serikali
sikuzote ipo bega kwa bega na waandaaji wa mashindano haya katika
kuhakikisha kwamba hayakwami na iko tayari kusaidia kwa hali na mali
ili yaweze kufanyika kwa kiwango cha kimataifa.
Imetolewa na,
Mratibu Matukio,
Hamis .A. Mkongowale
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)