Rais Kikwete atunuku Nishani Ikulu wakati wa Sherehe za miaka 51 ya Uhuru - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Rais Kikwete atunuku Nishani Ikulu wakati wa Sherehe za miaka 51 ya Uhuru

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku  nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani leo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue ,Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude) Pichani juu.Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari jeshi na polisi
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.
  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam,(katikati)Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi.

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akivishwa nishani baada ya kumvisha nishani yake leo

Rais Jakaya Kikwete akimvisha nishani Balozi Ombemi Sefue  ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi ikulu leo jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages