RAIS KIKWETE AKABIDHI NYUMBA MPYA 35 ZA WALIOATHIRIKA NA MILIPUKO YA MABOMU YA GONGO LA MBOTO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE AKABIDHI NYUMBA MPYA 35 ZA WALIOATHIRIKA NA MILIPUKO YA MABOMU YA GONGO LA MBOTO

Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012.
Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga nyumba mpya 35 kwa ajili ya waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya duka.
Baadhi ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekana leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages