Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama
hicho Mwigulu Nchemba wakirejea jukwaani mara baada ya kuwatunza watoto
hao Nyambuli na Gozbert wakati wakicheza ngoma katika maadhimisho ya
miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akionyesha uwezo wake katika kupiga ngoma huku akiwa amelala chini katika maadhimisho hayo.
Ukiangalia
katika picha hii utawakumbuka watoto hawa Nyambuli Mganga (5) na
Gozbert Bwere (3) kutoka mkoani Mara ambao walikuja jijini Dar es salaam
na kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani humo, kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja
wa Uhuru, watoto hawa walitia fora sana mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Bara Dk. Jakaya Kikwete na
wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi waliohudhuria katika
maadhimisho hayo.
Shughuli kubwa iliyofanywa na
mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya
baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo,
ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu
Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba walienda na kumtunza mtoto huyo
kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.
Jana nilipita maeneo ya Manzese
katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa
wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli hiyo, akajitambulisha
kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni msaidizi wa Afisa Utamaduni wa
Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na kikundi hicho kama
mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.
Kilichinisikitisha sana ni
kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa ya pombe kali aina ya Value
akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko cha chupa
hiyo, huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa pombe
hiyo ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kuinywa.
Kitu kilichiniumiza sana
nilipoongea na Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto
hao wamebaki Musoma. Hivyo watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi
hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano mkubwa wa
kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa kotosha
kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe hiyo ya Value na
kiongozi huyo.
(NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)