Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete akizungumza kwenye ufunguzi wa semina hiyo jana. Katika maneno yake ya ufunguzi alisema lengo kuu la semina hiyo ni kuimarisha chama kiweze kushika dola kwa kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisema Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake bila ya msukumo kutoka katika chama, aliwataka viongozi katika ngazi zote kuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli za maendeleo badala kukaa tu ofisini na kuagiza walio chini yao.
Kiongozi wa wakufunzi wa semina hiyo Ndugu Lukasi Kisasi akijitambulisha kwa wajumbe wa semina hiyo.
Baadhi ya madiwani waliohudhuria semina hiyo wakiskiliza kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo, jumla ya madiwani 64 wameshiriki kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza katika Semina hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wajumbe wa
semina elekezi ya madiwani wa CCM wa Mkoa wa Rukwa wakati akifunga
semina hiyo iliyoanza jana na kumalizika leo katika ukumbi wa Manispaa
ya Sumbawanga. Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Kushoto
ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete.
Semina hiyo iliyokuwa ya mafunzo ilikuwa na lengo la kuimarisha utendaji
kazi wa chama hicho pamoja na kukiongezea chama uwezo zaidi wa
kuisimamia shughuli za Serikali katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
wa chama hicho pamoja kukiongezea nguvu zaidi kiweze kushinda katika
uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
Semina
hiyo ilikuwa na jumla ya mada tisa amabazo ni historia ya CCM tangu
TANU na ASP, Katiba ya CCM ya mwaka 1977-2012, Sera za msingi za CCM,
Muelekeo wa Sera za CCM mwaka 2010-2020, Sera za Umma, Utekelezaji wa
sera Ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea katika mazingira ya utandawazi na
uchumi wa soko, Hali ya kisiasa na mikakati wa ushindi kwa ajili ya
uchaguzi Mkuu 2015, Uandishi wa katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania na Majukumu yatokanayo na taarifa ya kazi na maazimio ya
Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)