Mkurugenzi
wa Tahmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA)
wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bw.Ignace Mchallo akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari kwa niaba
ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ambapo amesema Wizara imetoa agizo la kufanya
ziara katika Viwanda vilivyopo eneo la Mikocheni na fukwe za hoteli
zilizoko katika bahari ya Hindi maeneo ya Manispaa ya Kinondoni kujionea
changamoto za uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambayo huleta
athari kwa jamii kwa ujumla. Katikati ni Mkuu wa Msafara Naibu Waziri wa
Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na
kulia ni Mkemia Mkuu wa Mazingira katika Ofisi hiyo Bi. Rogathe Kisanga.
Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert
Ntakamulenga kutoka NEMC akitoa maelezo kwa Naibu Waziri ambapo amesema
NEMC imetoa agizo kwa wamiliki wa Viwanda kuhakikisha wanafunga mitambo
maalum yakusafisha maji taka yatokanayo na bidhaa wanazozitengeneza hasa
zinazotumia rangi kabla ya kuyamwaga katika mifumo ya maji machafu ili
kupunguza athari za uharibu wa mazingira.
Naibu
Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga akizngumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza ziara ya
kukagua Viwanda na Mahoteli yaliyopo maeneo ya fukwe za bahari ya Hindi
jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Watanzania kuzijua na kuzifwata
sheria za Mazingira ikiwemo sheria ya mwaka 2004 namba 20 inayowataka
watu kutunza mazingira yanayowazunguka.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akitoa ufafanuzi kwa Naibu
Waziri kuhusiana na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kisheria kwa watu
wanaochafua mazingira wakiwemo wanaomwaga maji machafu yenye kemikali
zinazoharibu Mazingira kutoka viwandani wakati wa ziara ya kukagua Mto
Mlalakuwa uliopo maeneo ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Huu ndio Mto Mlalakuwa Kawe Darajani unavyoonekana ambapo maji yake yanaonyesha kuchafuliwa na maji taka yatokayo viwandani.
Mkurugenzi
wa Tahmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA)
wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bw.Ignace Mchallo akifafanua jambo kwa Mh. Charles Kitwanga wakati wa
ziara hiyo sambamba na jopo la waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali.
Eneo la Mto Mbezi lenye mgogoro kufuatia kuzuia mtiririko wa maji ya Mto
huo ambalo limenunuliwa na mtu Binafsi anayefahamika kwa jina la Robert
Mgishwagwe ambaye kila anapofuatwa na vyombo husika kumtaafiru kwamba
eneo hilo haliruhusiwi kujengwa amekuwa akikaidi na kudai kwamba yeye ni
mfanyakazi wa Usalam wa Taifa. Kitendo cha kuweka Kifusi na
kukisawazisha katika njia ya maji ya mto Mbezi na kimesababisha Daraja
lililopo kando ya eneo hilo kuvunjika kila mara na kusababisha usumbufu
kwa wananchi.
Naibu
Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga akikagua eneo la kiwanja cha mtu huyo kinachosababisha usumbufu
kwa wananchi na kutoa agizo kwa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira pamoja na maafisa wa Wizara yake kuhakikisha hatua za kisheria
zinachukuliwa mara moja dhidi ya mtu huyo.
Msafara wa Mh. Charles Kitwanga ukiwasili eneo la Viwanda Mikocheni jijini Dar es Salaam tayari kwa ziara ya Ukaguzi.
Pichani
Juu na chini ni Mheshimiwa Naibu Waziri Charles Kitwanga (katikati)
kipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kuratibu Miradi wa kiwanda cha
MM I Steel Bw. Lawrance Manyama (kushoto) wakati alipofanya ziara rasmi
kuangalia changamoto za uharibu wa mazingira unaotokana na Viwanda na
Mahoteli. Kulia ni Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga.
Mh.
Charles Kitwanga katika ziara ya ghafla katika kiwanda cha MMI Steel
akikagua moja ya shimo la maji taka katika kiwanda hicho ambapo
ameuagiza utawala wa Kiwanda hicho kuingia katika makubaliano maalum na
NEMC katika siku chache zijazo kuhakikisha wamefunga mitambo maalum ya
kutibu majibu taka yenye kemikali za kutoka viwandani mwao kwa kiwango
kinachokubalika kitaifa.
Meneja Mkuu wa kiwanda cha TANPACK TISSUES Ltd. Bw. Rajesh Shah akitoa
ufafanuzi kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga kuhusiana na kiwanda chake kuwa
na mikakati ya kuhakikisha maji taka yatokanayo na uzalishaji kiwandani
humo hayataleta madhara kwa jamii.
Mh. Charles Kitwanga akikemea vikali tabia ya uchelewashwaji wa maagizo
yanayotolewa na Serikali wakati wa ziara yake katika Kiwanda hicho
sambamba na viongozi wa NEMC.
Meneja Mkuu wa kiwanda cha TANPACK TISSUES Ltd. Bw. Rajesh Shah
akimuonyesha Mh. Naibu Waziri Charles Kitwanga sehemu maalum ya kuchujia
maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho.
Meneja
Mkazi wa Kampuni ya BIDCO inayotengeneza mafuta ya kula na sabuni Bw.
Hemal Shah akimuogoza Mh. Kitwanga kukagua tenki linalohifadhi uchafu
baada ya kutengeneza sabuni ambao pia husafishwa kitaalamu kupunguza
kemikali zilizomo ndani yake.
Pichani Juu na Chini Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akikagua matenki hayo wakati wa ziara
hiyo aliyoambatana na wanahabari pamoja na viongozi wa NEMC.
Maafisa wa Wizara, NEMC na baadhi ya wanahabari wakiangalia taratibu
zinazopitiwa kupitisha na hatimaye kusafisha maji taka ya viwanda kabla
ya kwenda kuyamwaga katika maeneo ya wazi.
Naibu Waziri Mh. Kitwanga akitoa agizo kwa Uongozi wa BIDCO wakati wa ziara ya kukagua viwanda mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha awamu
ya kwanza ya ziara ya kutembelea viwanda vya jijini Dar es Salaam ambapo
amesema ziara hiyo imempa nafasi ya kujionea hali halisa ya viwanda vya
jijini na kugundua kuwa vingi havina mitambo ya kusafisha maji machafu
yanayokwenda kumwagwa kwenye mito na kushuhudia kuwa vingine havina
viwango vya kupeleka maji taka yake kwenye mtandao wa maji taka ya
DAWASCO na kuwataka kufikia viwango vinayokubalika na mazingira yetu.
Msafara
wa Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.
Charles Kitwanga ukiondoka mara baada ya kumaliza ngwe ya kwanza ziara
ya Kukagua Viwanda kuangalia hali halisi jinsi viwanda hivyo vinafuata
kanuni za utunzaji mazingira.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)