Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati
alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya
Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba 23, 2012. Mzee huyo
anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 13.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na
wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo
Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa
ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal.
Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka,
Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo
cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea ramani ya ujenzi mpya wa shule ya Chwaka, kutoka kwa Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Fadhili Hamada Mshamba, wakati alipotembelea
kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC)
leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya
Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya
kituo hicho leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mzee Silima Jendele, wakati
Makamu alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Wazee leo, katika Mkoa
wa Kusini Unguja.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)