Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar asimamia kumaliza mgogoro wa maeneo ya kilimo katika vijiji vya Dole, Ngurueni na Ndunduke Dole - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar asimamia kumaliza mgogoro wa maeneo ya kilimo katika vijiji vya Dole, Ngurueni na Ndunduke Dole


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa maamuzi makali yaliyopelekea kuteua Kamati ya kusimamia kumaliza mgogoro wa maeneo ya kilimo katika vijiji vya Dole, Ngurueni na Ndunduke Dole mara baada ya kupokea kero za Wakulima hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishuhudia nyaraka bandia walizopewa baadhi ya watu walio nje kabisa ya maeneo ya kilimo ambapo Mkurugenzi wa Ardhi Nd. January Fusi alizibaini baada ya kuwasilishwa kopi zake na wakulima hao.Kati kati ya Balozi Seif na Ndugu January Fusi ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Alfan Othman aliyevaa kofia ya kiua.
Mwenyekiti wa kufuatilia matatizo ya wakulima wa Dole na Ngurueni Bwana Daudi Sirus Mukaka akiwasilisha maazimio yao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambayo walikubaliana katika vikao vya awali lakini hayajatekelezwa na hatiame kuleta kero.
Baadhi ya Wakulima wa Dole, Ndunduke, na Ngurueni Wilaya ya Magharibi wakiwa katika kikao cha kuwasilisha malalamiko yao ya kucheleweshewa kupewa umiliki wa maeneo ya kilimo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani hapo skuli ya Wazazi Dole.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages