Naibu mkurugenzi wa Idara ya Vijana Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na michezo James Kajugusi(katikati)akifungua
kongamano la wajasiriamali vijana la siku tatu linalofanyika kwenye
ukumbi wa Don Bosco vijana Upanga jiji Dar es salaamAmbapo amesema
vijana wengi wakiwa wajasiriamali nchi itazidi kuwa na amani mshikamano
na utulivu kwa sababu watatumia muda wao katika shughuli za kujiongezea
kipato na hivyo kuboresha maisha yao.tuna ziomba taasisi za fedha kuwapa
kipaumbele vijana ambao wana elimu ya ujasiriamali kwa kuwapa mikopo
yenye masharti nafuu.
Hii ni kwa sababu ya utaalamu na
ujuzi walionao ni rahisi kwa vijana wajasiriamali kufanya marejesho ya
mikopo waliopewa.Aidha kwa kuwa watakuwa wamekidhi vigezo vya
kisheria,usalama wa bidhaa zao utakuwa mkubwa zaidi kuliko wale
wanaofanya biashara kiholela na kwa kubahatisha.(kushoto) ni Ofisa Uhusiano wa Benki ya NBC Eddie Mhina.(kulia katikati)Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali inayojishughulisha na
uendelezaji wa wajasiriamali vijana Tanzania Bara( YESI) Bw. Denis
Maira(wakwanza kuli)Bw.Hassan Ngoma
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali inayojishughulisha na
uendelezaji wa wajasiriamali vijana Tanzania Bara( YESI) Bw. Denis Maira
akifafanua jambo kwenye kongamano hilo la wajasiriamali vijana
Wadau mbalimbali kutoka sekta za ujasiriamali wakifuatilia kwa umakini hotuba iliokuwa ikitolewa na Naibu mkurugenzi wa Idara ya Vijana Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na michezo ,James Kajugusi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)